Hawa Mbeya City ni nomaa
aisee, wameshika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya
kushinda bao 2-0 katika Mbeya Derby.
Kutokana na ushindi huo,
wamefikisha pointi 23 sawa na vinara Azam FC, hivyo kubaki katika nafasi ya
pili, huku wakiishusha Yanga inayorudi nafasi ya tatu na Simba ya nne.
Katika ‘Mbeya Derby’
iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, City wameonyesha kweli
wanaweza.
Mabao mawili yote yakifungwa
katika kipindi cha kwanza, yaliwaacha Prisons hoi.
Huku ikishangiliwa zaidi,
Mbeya City ya Juma Mwambusi ilipata bao lake la kwanza katika dakika ya 62
mfungaji akiwa Peter Mapunda.
Wakati Prisons wanajiuliza,
Deogratius Julius alifunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya
69.
Baada ya hapo, Prisons
waliendelea kuteseka huku City wakishambulia kama nyuki hadi mwisho wa dakika
90.
0 COMMENTS:
Post a Comment