October 8, 2013





Sasa kila kitu kimekuwa wazi kwamba Arsenal itaanza kutumia vifaa vya kampuni ya Puma.

Hilo limegundulika baada ya bingwa wa zamani wa Olimpiki katika riadha kutoka Uingereza, Linford Christie kuweka picha akiwa na wachezaji wawili wa Arsenal na mkongwe Thierry Henry.


Katika picha hiyo, Henry, Olivier Giroud na Bacary Sagna walikuwa wamevaa jezi za Arsenal zenye nembo hiyo ya Puma.

Dakika chache baada ya Christie kuiweka picha hiyo kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter, haraka aliifuta lakini hata hivyo akawa amechelewa na imeishavuja.
Mkataba mpya wa Arsenal na Puma ni wa miaka mitano na utagharimu pauni milioni 30 kwa mwaka.
Mkataba huo wa Arsenal na Puma unakuwa ghali zaidi hata kuliko ule wa Liverpool wa pauni 25 kwa mwaka na kampuni ya Warrior, maana yake huo wa Arsenal utakuwa juu zaidi.
Arsenal imefanya kazi na Nike kwa miaka 20, mkataba wa kwanza waliingia mwaka 1994 na mara ya mwisho waliingia mkataba wa miaka saba uliogharimu pauni milioni 55.
Manchester United pia wana mkataba wa miaka 15 na Nike ambao wataingiza pauni milioni 287 kwa muda wote huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic