October 8, 2013



OWINO NA KAZE MAZOEZINI


Beki wa kati wa Simba, Joseph Owino ambaye alikuwa na maumivu amerejea mazoezini leo.


Owino raia wa Uganda, amerejea mazoezini na kujiunga na wenzake katika kambi ya Simba iliyo katika eneo la Bamba Beach, Kigamboni jijini Dar.

Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema Owino amekuwa fiti na kufanya mazoezi na wenzake hii leo.

“Amefanya mazoezi pamoja nasi, hivyo atakuwa amerejea katika hali nzuri,” alisema.

Owino ni ‘roho’ ya safu ya ulinzi ya Simba kwa kushirikiana na Gilbert Kaze ‘demunga’ raia wa Burundi wamekuwa tegemeo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic