October 8, 2013


Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor Binslum amefiwa na baba yake mzazi aliyekuwa na umri wa miaka 78.
 
Katika ukuta wake wa Facebook, Binslum amewashukuru Watanzania wanaoishi katika mji wa Hyderabad kwa kushiriki mazishi ya mzazi wake huyo huyo ambaye alikuwa amempeleka kwa matibabu.

“Alhamdulillah mzee wangu kipenzi tumempumzisha katika maisha yake mapya kabisa ya kaburini masaa kadhaa yaliyopita jijini Hyderabad India, shukran kwa ndugu zangu wa Tanzania na Kenya wanaosoma huku kwani walinifanya nione msiba kama umetokea nyumbani tu.

“Lakini pia ndugu, jamaa na marafiki wote humu mulionesha kuguswa na msiba huu kwani maombi yenu kwa mzee wangu na wetu sijui hata nimjibu au kumshukuru nani kwa kuguswa na msiba huu,” aliandika Binslum na kumalizia.

“From my Heart nasema asanteni sana sana kunifanya nijione kumbe nyinyi ni familia yangu tusiyojuana baadhi yetu. Sioni cha kuwalipa the way mulivyonifariji ila niwaambie Allah ndiye mlipaji bora kabisa katika walipaji.”
Kabla ya msiba huo, Binslum alifantiwa upasuaji wa goti lake ingawa alisisitiza kilichompeleka nchini humo ni matibabu ya mzazi wake huyo.
SALEHJEMBE inatoa pole kwa familia ya Binslum

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic