Barcelona imeishinda Real Madrid kwa
mabao 2-1 katika mechi ya La Liga maarufu kama El Clasico.
Mshambuliaji Mbrazil, Neymar da Silver
amefunga bao la kwanza katika dakika ya 19 huku Alexis Sanchez aliyeingia
kipindi cha pili akimalizia kazi katika dakika ya 78 kutokana na makosa ya kipa
Diego Lopez.
Bao moja la wageni Real Madrid kwenye
Uwanja wa Camp Nou, lilifungwa katika dakika ya 90 na Jese Rodriguez aliyeingia
kipindi cha pili.
Mechi hiyo ilikuwa nzuri ingawa
wachezaji wawili nyota Cristiano Ronaldo na Lionel Messi walishindwa kuonyesha
cheche zao.
Lakini mshambuliaji ghali zaidi duniani,
Gareth Bale naye alishindwa kuonyesha cheche zake na kutolewa katika kipindi
cha pili.
Kutokana na ushindi huo, Barcelona
imekwea kileleni ikifuatiwa na Atletico Madrid yenye mchezo mmoja mkononi na
Madrid wako katika nafasi ya tatu.
VIKOSI:
BARCELONA: Valdés, Alves, Piqué,
Mascherano, Adriano, Sergio Busquets, Xavi, Iniesta (Song 77), Fàbregas
(Alexis 70), Messi, Neymar (Pedro 84)
WALIOBAKI BENCHI: Pinto, Montoya, Puyol, Sergi Roberto
KAZI ZA NJANO: Adriano, Busquets
WAFUNGAJI: Neymar 19, Alexis 78
REAL
MADRID: Diego López, Carvajal, Varane, Pepe, Marcelo, Ramos (Illarramendi
56), Modric, Khedira, Di Maria (Jese 76), Ronaldo, Bale (Benzema 61)
WALIOBAKI BENCHI: Casillas, Coentrão, Arbeloa, Isco
KADI ZA NJANO: Bale, Ramos, Khedira,
Marcelo
MFUNGAJI: Jese 90
0 COMMENTS:
Post a Comment