Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji Simba na Tanzania Prisons kutoka
Mbeya iliyochezwa jana (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 60,521,000.
Simba
iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi hiyo namba 55 na kushuhudiwa na
watazamaji 10,494 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh.
15,000 na sh. 20,000.
Kila
klabu ilipata mgawo wa sh. 14,191,002.55 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 9,232,016.95.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,215,763.96, tiketi sh.
3,183,890, gharama za mechi sh. 4,329,458.37, Kamati ya Ligi sh. 4,329,458.37,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,164,729.19 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,683,678.26.
0 COMMENTS:
Post a Comment