BENCHI LA UFUNDI: KOCHA MKUU, Kibadeni, MSAIDIZI WAKE, Julio, MENEJA, Nico Nyagawa na KOCHA WA MAKIPA, James Kisaka. |
Kiungo mkongwe wa Simba, Henry Joseph
ataendelea kubaki timu katika timu ya pili, huo ni uamuzi wa benchi la ufundi la timu hiyo.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo
amesema Henry atabaki hapo hadi atakapobadilika.
“Anatakiwa kubadilika na kuonyesha
juhudi, kwamba alikuwa anacheza nje basi atuonyesha kweli anastahili kuwa
katika timu ya kwanza na atatoa msaada.
“Sisi hatujapenda vyimbo vya habari
ambavyo vimeandika tofauti kama vile kufukuzwa Simba na vinginevyo,
tulichofanya sisi ni kwa manufaa ya Simba.
“Kama Henry anagekuwa anajituma wala
kusingekuwa na tatizo, tunajua alikuwa Ulaya na ndiyo maana tunategemea mchango
mkubwa kutoka kwake. Tofauti tunaona si sahihi,” alisema Julio.
Henry alizuiwa kuendelea na mazoezi na
Kocha Mkuu, Abdallah Kibadeni baada ya yeye kuanza kuomba apumzike.
Kibadeni alimueleza aendelee kupumzika
baada ya kiungo huyo kurudi uwanjani na kutaka kuendelea na mazoezi.
Kabla ya hapo, Henry aliomba kupumzika kwa
madai alikuwa amefanya mazoezi binafsi hivyo kuusikia mwili hauna nguvu.
Lakini ilielezwa alijichanganya kwani
awali alimwambia Julio anajisikia ni mgonjwa halafu akamueleza Kibadeni kwamba
alikuwa amechoka kutokana na mazoezi.
Kibadeni akamueleza akendelee kupumzika
kwenye gari kama alivyokuwa amekaa hapo awali.
0 COMMENTS:
Post a Comment