October 11, 2013


Benchi la ufundi la kikosi cha Simba, limetamka kuwa tumu yao ipo kamili kabla ya kuwavaa Maafande wa Magereza, Tanzania Prisons ya Mbeya kesho, lakini ukatoa tahadhari juu ya jambo moja.


Kocha Msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwelo ‘Julio, ameiambia Salehjembe kuwa timu yao imefanya maandalizi ya kutosha katika kuelekea katika mchezo wa kesho, utakaopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, ambapo wataingia wakiwa na lengo moja, kusaka pointi tatu muhimu.

Julio, amesema kila mchezaji wa timu hiyo, inayoongoza ligi ikiwa na pointi 15, baada ya kushuka dimbani mara saba, yupo katika hali nzuri, lakini wanahofia taarifa za wapinzani wao wa jadi Yanga, kuwaharibia mipango yao hiyo, kufuatia kuwepo kwa taarifa za kupanga mikakati ya kukihujumu kikosi cha Wekundu hao.

“Hatuna tatizo kila kitu kinakwenda vizuri, tumefanya maandalizi ya kutosha, hatuna majeruhi yoyote katika kikosi chetu, tunawaheshimu wapinzani wetu Prisons, tutaingia uwanjani kutaka pointi tatu muhimu, ingawa tunajua kuwa soka ina matokeo ya aina tatu,” alisema Julio na kuongeza:
“Mchezo wa soka una mambo mengi, wakati mwingine fitina hazikosekani na hivi sasa, kuna taarifa nyingi kuwa wapo wapinzani wetu wana nia ya kutaka kutuharibia mipango yetu, lakini Simba ipo imara kupambana na kila changamoto.  

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic