Kocha wa Azam FC, Stewart Hall
amezichambua Simba na Yanga, lakini akaeleza sababu mbili zitakazokinufaisha
kikosi cha Yanga katika mchezo baina ya timu hizo keshokutwa Jumapili kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar.
Stewart ameliambia gazeti hili kuwa,
vikosi vya Simba na Yanga vina tofauti kubwa, ambapo Wekundu hao bado
hawajafanikiwa kucheza vema, jambao ambalo vinaweza kuwapa wakati mgumu katika
mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara.
“Timu zote ni nzuri, lakini Simba naiona
kama mpya yenye vijana wengi na kocha mpya, mpaka sasa bado hawajaweza kufikia
ubora ule unaotegemewa na wengi,” alisema Stewart na kuongeza:
“Ukiiangalia Yanga wachezaji wao ni wenye
uzoefu mkubwa, lakini wapo pamoja kwa muda mrefu, kifupi ni kwamba wanajuana
vizuri, kama watatumia faida hiyo ndiyo nasema inaweza kuwapa matokeo mazuri
katika mechi hiyo.”
0 COMMENTS:
Post a Comment