Kila ifikapo Jumanne au
Jumatano ya kila wiki, mshambuliaji Mrundi wa Simba, Amissi Tambwe, anaugua.
Tambwe amekuwa
akilalamika kuumwa kila siku hizo mbili zinapofika na gazeti hili limefuatilia
kwa wiki tatu sasa.
Uchunguzi
uliofanywa na blogu hii umebaini kuwa, wiki tatu zilizopita aliugua tumbo, wiki
iliyofuata akawa wanasumbuliwa na malaria na juzi akawa anadai kusumbuliwa na
malaria tena.
Akizungumzia hali hiyo,
Tambwe alisema kuwa anahisi hiyo inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa
yanayotofautiana na kwao Burundi.
“Suala la siku labda
limetokea tu lakini nimekuwa nikiugua kila wiki kutokana na kubadili mazingira
ya hali ya hewa ya hapa nchini ambayo ninaona haijanipenda. Jana (juzi)
niliugua tena malaria, lakini nashukuru ninaendelea vizuri hivi sasa na mechi
ya Yanga nitacheza,” alisema Tambwe.
Mshambuliaji huyo
aliyejiunga na Simba akitokea Vital’O, ndiye nahodha wa timu ya taifa ya
Burundi na sasa anaongoza kwa upachikaji mabao Ligi Kuu Bara, anayo nane.
0 COMMENTS:
Post a Comment