Kampuni ya
mawasiliano ya Airtel Tanzania imetangaza ushirikiano na klabu ya mpira wa
miguu ya Manchester United ya nchini Uingereza utakaowezesha wateja wa kampuni
hiyo kujishindia safari za kwenda kushuhudia mechi za klabu hiyo moja kwa moja
(live) katika uwanja wa Old Trafford.
Ushririkiano
huo ulienda sambamba na uzinduzi wa promosheni ya kampuni hiyo ijulikanayo kama
‘Mimi Ni Bingwa’ inayolenga kuwazawadia wateja zaidi ya shilingi milioni 500.
Akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni hiyo jijini Dar es Salaam leo,
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso alisema ubia huo mpya
unadhihirisha nia ya kampuni ya kufurahisha na kutoshereza mahitaji ya wateja
wake.
MKURUGENZI WA MICHEZO, LEONARD THADEO AKIZUNGUMZA (KUSHOTO) |
“Kampuni ya
Airtel Tanzania leo hii inatangaza rasmi kuingia ubia mpya ambao umelenga
kuwapatia wateja wetu fursa za kuangalia mechi za timu ya Manchester United
moja kwa moja(live) katika uwanja wa Old Trafford. Tunafuraha kushirikiana na
Manchester United, moja ya klabu kubwa katika historia ya mpira wa miguu
duniani.
Aidha,
mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa
Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na
Michezo, Leonard Thadeo wakati wa hafla hiyo aliipongeza kampuni ya Airtel kwa
kuendelea kusaidia maendeleo ya sekta ya michezo nchini.
RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI NAYE ALIZUNGUMZA |
UJUZI |
COLASO AKIMKABIDHI JEZI THADEO, MALINZI ANASHUHUDIA |
“Nachukua nafasi hii kuishukuru kampuni ya
Airtel Tanzania kwa jitihada zake za kuendelea kusaidia maendeleo ya michezo
nchini hususani Airtel Rising Stars ambayo imeibua vipaji kama Serengeti Boys
na Timu ya Tanzanite kwa wasichana ambao wamekuwa wakiiwakilisha nchi vizuri
katika michezo ya kimataifa,” alisema Thadeo.
0 COMMENTS:
Post a Comment