November 11, 2013


Al Alhy imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika baada ya kuichapa Orlando Pirates kwa mabao 2-0.


Timu hiyo kongwe ya Misri sasa imetwaa ubingwa kwa mara ya nane.

Katika mechi ya awali, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini. Kwa ushindi wa leo maana yake Al Ahly imeshinda kwa jumla ya mabao 3-1.

Bao la kwanza la Ahly lilifungwa na mkongwe Mohammed Aboutrika kabla ya Ahmed Abdel Zaher hajamalizia kazi.


Hata hivyo Orlando Pirates ilijitahidi kupambana ili kuibwaga timu hiyo kongwe kutoka Afrika Kaskazini lakini hakukuwa na mabadiliko.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic