November 11, 2013

 
AFIF (KULIA) AKIWA NA ZAMOYONI MOGELLA WAKATI WAKIWA SIMBA PAMOJA

Kocha wa zamani wa Simba, Hassan Afif yuko nchini Hispania ambako ameamua kujiendeleza zaidi.


Akizungumza kutoka Hispania, Afif ambaye sasa anafanya kazi zake nchini Qatar amesema tayari ameanza masomo.

“Nitakuwa huku kwa miezi sita, nimeamua kujiendeleza zaidi kwa kuwa dunia inakwenda kwa kasi.

“Soka ya sasa kila siku mambo mapya na tunachojaribu ni kupambana vilivyo na kujiendeleza pia,” alisema.

Afif alipata umaarufu mkubwa akiwa kocha mchezaji wa Simba, mara nyingi alikaa kwenye benchi na kila alipoingia alitoa pasi iliyozaa bao na hasa kwa mshambuliaji Zamoyoni Mogella.

Pamoja na kuwa mtoaji mzuri wa pasi zilizozaa mabao, Afif pia alikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga mabao muhimu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic