November 3, 2013




Pamoja na kuondolewa kazini, aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah ataendelea kulipwa mshahara.


Kwa mujibu wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi, katibu huyo wa zamani ataendelea kulipwa mshahara kwa muda huo ambao ndiyo mkataba wake utamalizika.

“Ataendelea kupata haki kama kawaida na baada ya hapo tutakuwa tumemalizana,” alisema.

Kuhusiana na Boniface Wambura ambaye amepewa nafasi ya kukaimu nafasi hiyo Osiah, Malinzi amepomba apewe ushirikiano.


“Kamati ya Utendaji inaziomba klabu, vyama vya wilaya, vyama vya mikoa, vyama shiriki na wadau wote kumpa ushirikiano Boniface Wambura katika utekelezaji wa majukumu yake,” alisema Malinzi leo asubuhi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic