November 27, 2013





Arsenal imezidi kupaa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Marseille kwa mabao 2-0.
 
Mabao yote ya Arsenal yamefungwa na Jack Wilshere ambaye aling’ara katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Emirates mjini London.


Katika mechi nyingine, Mohammed Salah wa Basle akaendeleza ubabe wake kwa Chelsea kwa kufunga bao pekee na kikosi cha Jose Mourinho kikalala kwa bao 1-0.


Wababe wengine Barcelona wakiwa ugenini wakakumbana na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ajax.

AC Milan nao wakazinduka kwa ushindi we mabao 3-0 wakiwa ugenini dhidi ya Celtic na Balotelli na Kaka kila mmoja akitupia  bao moja.

Borussia Dortmund waliofungwa na Arsenal waliofungwa na Arsenal mechi iliyopita wakaamka na kuichapa Napoli kwa mabao 3-1.

Schalke wakiwa ugenini wakalazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya Steau Bucharest, Zenit nao wakalazimishwa sare ya 1-1 na wageni wao Atletico Madrid huku FC Porto waliokuwa nyumbani wakafanya kazi ya ziada pia kupata sare ya bao 1-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic