November 1, 2013



Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema kikosi chake kingeweza kuichapa JKT hata mabao sita kama kingekuwa makini.


Hata hivyo akasema amefurahishwa na ushindi wa mabao 4-0 katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, leo.

“Ilikuwa mechi ambayo timu yangu ilikuwa imebadilika kiuchezaji kama utalinganisha na mechi zilizopita, tulicheza vizuri.

“Lakini tatizo kubwa tulishindwa kutumia nafasi tulizozipata, ndiyo kitu muhimu ambacho tunapaswa kukifanyia kazi ili kuendelea kujikita kileleni.

“JKT walikuwa wazuri, hilo hatudharau lakini kikosi change kilicheza vizuri zaidi katika mechi ya leo,” alisema Brandts.

Mabao manne ya Yanga katika mechi ya leo yalifungwa na Mrisho Ngassa (mawili), Oscar Joshua na Jerry Tegete.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic