MASHABIKI WA SIMBA CHINI, WAKIWA NA WATANI ZAO YANGA (JUU) |
Mashabiki Simba wamepiga kelele na
kutala benchi lao la ufundi libadilike na kuwarudisha wachezaji wakongwe.
Zaidi ya mashabiki waliotuma ujumbe
mfupi kupitia barua pepe na wale waliopiga simu ya mkononi ya SALEHJEMBE, wamemtaka
Kocha Mkuu, Abdallah Kibadeni na wasaidizi wake kufikiria na kugeuza misimamo
waliyonayo.
“Kweli Kibadeni anatuangusha, ni kocha
mkongwe lakini anaonyesha hana msimamo, ninahisi anaburuzwa na watu wengine
maana anatoa uamuzi ambao unaonyesha kuna chuki. Wakongwe warudishwe,” alisema
Mohammed Kassim.
Juma Mroki, Thomas Mapunda
waliojitambulisha wanaishi Dar es Salaam na Songea, walisema wakongwe ndiyo
tatizo la timu hiyo.
“Angalia tumeongoza hadi dakika ya 90,
lakini tumeshindwa kujilinda. Uzoefu pia ni jambo muhimu, wakongwe
wasidhalauriwe eti kwa kuwa tuna vijana.”
Baadhi ya wachezaji wakongwe wa Simba
ambao wameshushwa kikosi cha pili ni Henry Joseph na Ramadhani Chombo ‘Redondo’.
Lakini mshambuliaji mwenye kasi, Haruna
Chanongo, naye ameshushwa kikosi cha pili kwa kuwa tu alishindwa kucheza vizuri
mechi moja dhidi ya Yanga!
Mashabiki Simba, jana walifanya vurugu
baada ya timu yao kushindwa kulinda bao na Kagera wakasawazisha katika dakika
za nyongeza.
Walifanya vurugu na kuvunja viti huku
baadhi yao wakiumia baada ya askari polisi kupambana nao wakati wakijaribu
kuzuia vurugu hizo.
Simba imekuwa ikisonga kwa mwendo wa
kusuasua na kusababisha kuendelea kuporomoka na sasa iko katika nafasi ya nne
baada ya Yanga walioshika usukani leo, Azam FC na Mbeya City.
0 COMMENTS:
Post a Comment