November 9, 2013



Nusura rekodi ya Kocha Jose Mourinho kutofungwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge ivunjwe, lakini bahati nasibu, Chelsea ikawawazisha kwa mkwaju wa penalti katika dakika za majeruhi.


Penalti hiyo ilipatikana baada ya Ramires kuangushwa na Eden Hazard akafunga na kufanya matokeo kuwa 2-2.

Lakini kabla ya hapo, kila mtazamaji au msikilizaji wa mechi hiyo alijua Wes Brom wameilaza Chelsea kwa 2-1.

Wachezaji wa Wes Brom walipinga penalty hiyo kwamba Mbrazil huyo alijiangusha, lakini mwisho hakukuwa na ujanja, ikapigwa.
Wageni hao walipata mabao yao kupitia kwa Shane Long (Dk 61) na Sessegnon (Dk 68, hii ikiwa ni baada ya Chelsea kuongoza kwa bao la Samuel Eto’o katika dakika ya 45.


%%%
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta (Mikel 73), Ramires, Lampard (Ba 64), Willian, Oscar (Mata 73), Hazard, Eto'o. 
Subs not used: Cole, Luiz, De Bruyne, Schwarzer.


West Brom: Myhill, Reid, McAuley, Olsson, Ridgewell, Yacob, Mulumbu, Amalfitano (Popov 89), Sessegnon (Morrison 81), Brunt, Long (Anichebe 79).
Subs not used: Luke Daniels, Vydra, Dawson, Berahino.

Referee: Lee Probert.










0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic