November 7, 2013

IVO AKIWA MAZOEZINI KWENYE UWANJA WA CITY JIJINI NAIROBI, LEO ASUBUHI

Na Saleh Ally, Nairobi
Kipa wa Gor Mahia ya Kenya, Ivo Mapunda amesema amekuwa maarufu sana jijini hapa hata kuliko ilivyokuwa jijini Dar.

Akizungumza jijini hapa, Ivo amesema amekuwa akipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wa Gor Mahia.
“Ninaishi vizuri sana hapa, ninaelewana na watu wengi na kweli nimekuwa maarufu mno.

Watu wananiamini na tunaheshimiana sana, ninaishi maisha mazuri na nina furaha sana,” alisema Ivo katika mahojiano maalum.

Katika mitaa ya Nairobi, Ivo amekuwa maarufu sana kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha.

Msimu huu ameisaidia Gor Mahia kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Kenya ikiwa ni zaidi ya miaka 10 tokea walipoubeba kwa mara ya mwisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic