Michuano ya
Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu
za Ligi Kuu inaanza kutimua vumbi Novemba 17 mwaka huu katika viwanja vya
Karume na Azam Complex, Dar es Salaam.
Droo ya michuano hiyo
inayodhaminiwa na Maji Uhai imefanyika leo (Novemba 8 mwaka huu) mbele ya
waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
ambapo timu zimepangwa katika makundi matatu.
Kundi A linaundwa na timu za Azam,
Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Mbeya City na Yanga, wakati kundi B ni Ashanti
United, Mgambo Shooting, Oljoro JKT na Ruvu Shooting. Kagera Sugar, Mtibwa
Sugar, Rhino Rangers na Tanzania Prisons ndizo zinazounda kundi C.
Mechi za ufunguzi kundi A Novemba
17 mwaka huu ni kati ya Azam na Coastal Union (saa 2 asubuhi- Karume), Yanga na
Mbeya City (saa 8 mchana- Karume). Kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United
(saa 4 asubuhi- Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10 jioni- Karume).
Kagera Sugar na Mtibwa Sugar (saa
2 asubuhi- Azam) na Rhino Rangers na Tanzania Prisons (saa 10 jioni- Azam)
ndizo zitakazocheza mechi za ufunguzi Novemba 17 mwaka huu katika kundi C.
Robo fainali ya michuano hiyo
itachezwa Novemba 24 na 25 mwaka huu wakati nusu fainali itapigwa Novemba 26 na
27 mwaka huu. Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na ile ya fainali zitachezwa
Novemba 30 mwaka.
0 COMMENTS:
Post a Comment