November 4, 2013


Kamati ya utendaji ya Simba ilikutana jana jioni na kujadili masuala kadhaa likiwemo la kubaki au kuondoka kwa kocha msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.


Taarifa zinaeleza kwamba huenda Julio akafutwa kazi kutokana na kuonekana analalamikiwa sana na wachezaji.

Taarifa zinaeleza huenda Julio akaondoka Simba mara tu baada ya mechi ya mwisho ya Simba katika mzunguko wa kwanza.

“Sidhani kama Julio atarudi katika mzunguko wa pili, lakini ni suala ambalo linaendelea kujadiliwa,” kilieleza chanzo.


Julio ni msaidizi wa Abdallah Kibadeni na taarifa zinaeleza pia alijadiliwa katika kikao hicho lakini bado hakukuwa na jibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic