Na
Mwandishi Wetu, Songea
Bonanza kubwa la NANI MTANI JEMBE ambalo huenda jamii ya Mkoani Ruvuma inaweza kuliita
la kihistoria, limefanyika katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea limefanyika
jana, ambapo mamia ya wananchi walifurika kwa wingi uwanjani hapo huku
mashabiki wa Yanga wakishinda pambano la soka kwa mabao mawili na shindano la
kumsaka na kumkimbiza kuku wa kienyeji huku Simba wakiibuka kidedea kwenye
mchezo wa kuvuta kamba.
Hali
katika uwanja wa Majimaji, maarufu kama wanalizombe ulianza kufurika majira ya
saa nne asubuhi, baada ya wananchi hao wengi wakiwa vijana kumaliza shughuli za
ibada kutoka makanisani.
Mratibu
wa tamasha hilo kwa niaba ya Kilimanjaro Premium Lager, Amedeo Thadeo, alisema
kwamba wameamua kufanya bonanza hilo katika mji wa Songea baada ya kubaini kuwa
mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa yenye mashabiki wengi wa vilabu vya Simba
na Yanga.
Hata
hivyo, michezo kadhaa iliyoanza kufurahisha wananchi waliofurika katika uwanja
huo ulikuwa wa kufukuza kuku tena Jogoo, ambapo washiriki wawili wapenzi wa
klabu za Simba na Yanga walishirikishwa baada ya kuvalishwa jezi za vilabu
hivyo.
Lakini
kwa bahati mbaya, wapenzi wa Simba, walishindwa kuongeza furaha yao katika
uwanja huo, baada ya mshiriki wao kushindwa kumaliza mbio hizo kwa mafanikio,
huku yule wa Yanga Deogras Mwanji, akiibuka kidedea baada ya kufanikiwa
kumkamata jogoo huyo baada ya dakika mbili na sekunde 25.
Hata
hivyo, Mwakilishi wa Mauzo TBL mkoani Ruvuma Masoud Mrisho, aliliambia gazeti
hili kwamba mwamko ulikuwa mkubwa uwanjani hapo, baada ya vijana walikuja
kutoka Dar es Salaam kufanya maonyesho ya promosheni kadhaa kwenye baa kadhaa
mjini Songea.
“Walipokuja
hapa Songea wasanii waliosimamia bonanza hili walianza na kuendesha promosheni
katika baa ya Serengeti, Yapenda Mtini, Delux II, Mamboleo na kumalizia katika
baa ya VALONGO VANGU, mjini Songea na kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa
jamii,” alisema Masoud.
Masoud
alisema wananchi wengi walikuwa na shauku kubwa la bonanza, hivyo kila kona
alikopita yeye na wenzake, walitakiwa kuwahakikishia kwamba bonanza hilo
litafanyika bila kukosa, huku wanenguaji kutoka Bendi za Akudo Impact
Chicharito, na Afande aka Mjeda na Queen Lucy aka Mama Mdogo wakilipamba jukwaa
na kuwaburudisha ipasavyo wananchi waliofurika uwanjani hapo.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili, umebaini kwamba shughuliza kijamii katika mji wa
songea zilisimama kwa muda kutokana na bonanza hilo, hali ambayo ilionyesha
kuwa wananchi wengi walikuwa na shauku kubwa na bonanza hilo, japo kuwa wasanii
wenyeji wa mji wa Songea walishindwa kuonyesha umakini wao baada ya kupatiwa
nafasi ya kusherehesha jukwaa.
Waliozungumza
na gazeti hili waliipongeza Kilimanjaro Premium Lager kwa bonanza hilo na
kusema limeamsha hamasa ya kimichezo mkoani humo, ambayo imepotea baada ya timu
ya Maji Maji iliyokuwa ikishiriki Ligi Kuu ya Tanzania kwa miaka kadhaa, lakini
ikajikuta ikishushwa daraja baada ya kushindwa kufanya vizuri.
Bonanza
hilo lililoshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Joseph Mkirikiti, alionyesha
dhahiri ni mshabiki wa Yanga, alipoingia uwanjani alikabidhiwa jezi ya klabu ya
Yanga, na aliamua kusalimia wananchi wote kwa kluzunguka na kupunga
mikono na kuamua kwenda moja kwa moja kukaa katika jukwaa kuu la
uwanja huo, na kuwapongeza wananchi waliojitokeza katika bonanza hilo akisema
amefurahishwa na uratibu wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa shughuli hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment