November 29, 2013

TUNAJARIBU  TU




Bingwa wa dunia, Francis Cheka leo amenitembelea ofisini kwangu.
Pamoja na majukumu mengi ya gazeti la Championi nilimpa muda na tukazungumza na kujadiliana mambo kadhaa.
 
Urafiki na undugu wetu umeanza miaka kadhaa akiwa bondia wa ngumi za ridhaa.
Kanieleza mambo kadhaa, lakini kauli yake hii: “tusimlaumu Matumla kulalamika leo, wala tusione aliyatumia maisha vibaya.
“Mabondia hatulipwi vizuri na fedha nyingi tunamalizia katika maandalizi.
TUKIWA NA JOHN JOSEPH WA CHAMPIONI

AKIWA NA WILBERT MOLANDI WA CHAMPIONI

“Angalia mimi leo ni bingwa wa dunia lakini hakuna faida kubwa kwenye malipo. Hili suala linaniumiza sana kichwa kwa kuwa sitakuwa juu siku zote.
“Itafikia siku nitakuwa kama Matumla, hivyo vyama na mashirikisho ya ngumi yatupiganie.”
Hakika niliona ana hoja ya msingi na ninaona wahusika wanapaswa kuifanyia kazi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic