November 2, 2013


Kocha Patrick Liewig aliyewahi kuinoa Simba, amesema timu hiyo itaendelea kufanya vibaya.


Liewig raia wa Ufaransa, amesema Simba itaendelea kufanya vibaya kwa kuwa kikosi chake bado hakijawa imara lakini ajabu hata ushirikiano haupo.

“Nimeona Simba ikicheza, angalau hata msimu uliopita ilikuwa ina kiwango kizuri.

“Nilitegemea msimu huu kuwe na mabadiliko makubwa, lakini mambo ni tofauti. Nimekuwa nikisikia wanazozana na wachezaji wengine kushushwa daraja wakati wana uzoefu na wanahitajika.

“Huenda sijaelewa kinachoendelea, lakini itakuwa vizuri sana kama watadumisha zaidi ushirikiano na kutafuta njia ya kuyatatua matatizo ya ndani bila kuongeza misuguano.

“Ugomvi husababisha hofu na mwisho unajenga uoga, hivyo wanatakiwa kuwa makini,” alisema Liewig ambaye alirejea nchini kwa ajili ya kudai fedha zake.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic