November 2, 2013


Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema kuwa kikosi chake kiwe bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, basi wanahitaji kushinda mechi zote walizobakisha.


Brandts raia wa Uholanzi amesema hayo ndiyo malengo aliyoyaweka yeye na benchi lake la ufundi katika mechi hizo.

“Ili tujiwekee mazingira mazuri ya ubingwa, basi tunahitaji tushinde kila mechi tutakayocheza. Hayo ndiyo malengo tuliyojiwekea kwenye msimu huu, ninaamini hilo litafanikiwa kutokana na ubora wa kikosi changu na ushirikiano ninaoupata kwenye benchi langu la ufundi,” alisema Brandts.

Aidha, Brandts amesema kuwa alimpa nafasi ya kucheza kwa dakika 10 mshambuliaji Lusajo Reliants katika mechi dhidi ya Mgambo kwenye Uwanja wa Taifa, Jumanne wiki hii ili kuona kiwango chake, na kusisitiza kuwa ataendelea kumpa nafasi kidogo ili awe katika hali ya mchezo.

Kweli alifanya hivyo tena katika mechi ya jana wakati Yanga ilipoivaa JKT Ruvu na kushinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Ruvu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic