November 10, 2013


 Kipa mpya wa Yanga, Juma Kaseja alichelewa kusaini kwa takribani siku nne kutokana na suala la matangazo.

Kipingele kinachohusiana na matangazo ndani mkataba huo wa Yanga kilitakiwa kuondolewa.


Baada ya kukutana na kukubaliana, Kaseja aliomba mkataba wake kwanza ausome.

Lakini aliporudishwa, kipengele hicho bado kilikuwa hewani.
“Aliporudishiwa kile kipengele bado haikutolewa, ndiyo ma ana Juma alikuwa anajaribu kukwepakwepa.

“Lakini baadaye aliwaambia Yanga moja kwa moja kwamba anahitaji marekebisho ndiyo asaini na wao wakafanya hivyo walipokutana, kweli akasaidia.

“Sasa Juma ni mchezaji halali wa Yanga,” kilieleza chanzo.
Hata hivyo haikuwelezwa kipengele hicho kama kilikuwa kinamzuia Kaseja kufanya matangazo au la.


Kaseja ana mkataba na kampuni ya viwaywaji baridi ya Pepsi Cola.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic