November 30, 2013

Mwanamuziki maarufu wa kike, Shakira na kipenzi chake, beki wa Barcelona, Gerard Pique wamezidi kuonyesha kuwa penzi lao liko hai baada ya kujitokeza katika mechi ya mpira wa kikapu.


Mechi hiyo, timu ya Barcelona ilikuwa inacheza dhidi ya Fenerbahce Ulker Istanbul kwenye Uwanja wa Palau Blaugrana jijini Barcelona.

Wawili hao walionekana kuwa karibu na kujadili mambo kadhaa huku mkono wa Shakira ukiwa katika paja la mpenzi wake huo muda wote.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kwamba wako kwenye mfarakano ndiyo maana siku nyingi hawajaonekana pamoja.
Kutokea tena wakiwa wenye furaha, inaonyesha wazi ni kama jibu la waliokuwa wakieleza kwamba wako katika mtafaruku.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic