November 8, 2013


Hatimaye ile ngojangoja imepata majibu, Juma Kaseja amerejea Yanga kwa mara nyingine.



Kaseja ambaye ni kipa maarufu zaidi katika soka Tanzania kwa kipindi hiki, amesaini Yanga mkataba wa miaka miwili na kupewa kitita cha Sh milioni 40.

Kazi hiyo imemalizika leo hii alasiri na Juma, rasmi ataanza kuitumikia Yanga katika mzunguko wa pili.

Yanga imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa inaongoza na kufuatiwa na Azam FC na Mbeya City.

Awali Kaseja alikuwa asaini jana lakini uongozi wa Yanga ukataka kumpa Sh milioni 20 kumtangulizia, akagoma.
Baada ya mechi dhidi ya Oljoro ambayo Yanga ilishinda mabao 3-0, viongozi wake wakamuita ili kuisaini lakini akawaomba wakutane leo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic