AKIKABIDHIWA JEZI NA MWENYEKITI WA AZAM FC, SAID MOHAMMED |
Kocha mpya wa Azam FC Joseph Omog
hatimaye leo ametua rasmi jijini Dar tayari kwa kuanza kazi ya kukinoa kikosi
hicho.
Omog raia wa Cameroon ametua leo saa
3:00 asubuhi na Ndege ya Shirika la Kenya ambapo mara baada ya kuwasili
alipelekwa moja kwa moja katika ofisi kuu za timu hiyo zilizopo Mzizima na
kusaini mkataba wa miaka miwili.
Mara baada ya kusaini mkataba huo
Omog anayechukua nafasi ya Muingereza Stewart Hall alitambulishwa rasmi kwa
waandishi wa habari na mwenyekiti wa timu hiyo Said Mohamed ambaye alimtaja
kocha huyo kuwa ni kati ya makocha bora sita wanaopatikana Bara la Afrika.
AKIKARIBISHWA BAADA YA KUWASILI NA MENEJA WA AZAM FC, PATRICK KAHEMELE |
Mohamed maarufu kama Mzee Said amesema
Azam inafuraha kubwa kumpata Omog ambaye uongozi wa timu hiyo umeona ndiye
anayestahili kuchukua nafasi ya Stewart aliyesitisha mkataba mwezi uliopita.
Omog kwa upande wake kocha wa zamani
wa kikosi cha AC Leopards ya Congo Brazaville alionyesha kushangazwa na
mapokezi aliyoyapata ambapo amesema mara baad ya kusaini mkataba huo sasa kazi
yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inaoata mafanikio ndani ya uwanja.
Kivutio kikubwa katika ujio wa kocha
huyo ni kuja na mwanaye Henry Omog ambaye ni beki wa zamani wa Canon
de Yaunde huku akiwa ndiye meneja wa baba yake huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment