November 30, 2013

WAZIRI MAKAMBA AKIZUNGUMZA

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba amewasifu kampuni ya Azam Group na kusema anaamini Azam Media itafanya vizuri sana.


Akizungumza katika uzinduzi wa Azam TV jana kwenye hoteli ya Hayat jijni Dar, Januari ambaye ni mbunge wa Bumbuli alisema anaamini runinga hiyo itapata mafanikio makubwa.
WAKATI WA UZINDUZI

“Kila wanachokugusa Azam kinakubali na kupata mafanikio, ninaamini hata Azam TV itafanikiwa sana,” alisema.

“Tunawaamini Azam kwa kila wanachogusa, lakini kitu muhimu ni content, hivyo wajitahidi kuwa na vitu vinavyowagusa watazamaji wao na hasa Watanzania.
MMOJA WA WAKURUGENZI WA AZAM TV, YUSUF BAKHRESA (MWENYE SUTI) AKIWA KWENYE UZINDUZI HUO.

“Watu wamekuwa wakilaumu kwa kila kitu, lakini bado vitu vinaanzishwa kama unavyoona Azam TV inaanzishwa. Vizuri tukajivunia, kama walivyosema wenyewe hii ni runinga ya kimataifa inayotokea Tanzania,” alisema.

Kabla Azam TV ilizindua king’amuzi chake chenye chaneli takribani 50 ambacho kitakuwa kinalipiwa Sh 12,500 tu kwa mwezi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic