Adhabu ya Simba kutakiwa kulipa Sh
milioni 25 kutokana na mashabiki wake kung’oa viti kwenye Uwanja wa Taifa,
huenda ikaongezeka kwa kuwa mpaka sasa haijalipwa.
Moja ya adhabu ambazo zimezungumzwa ni
kuwa, kuna uwezekano wa kucheza mechi sita bila mashabiki.
Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho
la Soka la Tanzania (TFF), Saad Kawemba, alisema suala la Simba linatarajiwa
kujadiliwa na kamati ya nidhamu ya TFF ambayo bado haijaundwa.
Lakini amesisitiza kuwa, kabla ya
uamuzi wowote wa adhabu ya ziada, pande zote tatu; serikali, Simba na TFF,
zitakutana kwa ajili ya mazungumzo.
“Kamati ya Nidhamu ya TFF itakapoundwa
ndipo suala lao litakapojadiliwa zaidi ili kujua kama adhabu itaongezeka au
itapunguzwa, kwani hadi sasa kamati hiyo haijaundwa.
“Kwani yanaweza yakatolewa maamuzi ya
kucheza mechi sita bila mashabiki iwapo tutaona adhabu iliyotolewa awali
haitoshi kulingana na kosa lenyewe,” alisema Kawemba.
0 COMMENTS:
Post a Comment