Kikosi cha timu ya Taifa ya
wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) kimewasili salama jijini Maputo,
Msumbiji tayari kwa mechi ya marudiano ya raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia
itakayochezwa kesho (Novemba 9, mwaka huu).
Kwa mujibu wa kiongozi wa msafara
wa Tanzanite, Kidao Wilfred ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), timu hiyo chini ya Kocha wake
Rogasian Kaijage ilifanya mazoezi yake ya kwanza jana asubuhi.
Tanzanite itafanya mazoezi yake ya
mwisho leo (Novemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto ambao ndiyo
utakaotumika kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni kwa saa
za Msumbiji.
Nao wachezaji waliobaki kumalizia
mtihani yao ya kidato cha nne wameondoka leo saa 11 jioni kwa ndege ya LAM
wakiongozwa na naibu kiongozi wa msafara, Khadija Abdallah Nuhu ambaye ni
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA).
0 COMMENTS:
Post a Comment