Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wamepaa
kileleni mwa ligi kuu ikiwa ndiyo mwisho wa mzunguko wa kwanza.
Yanga imeshika usukani kwa kufikisha
pointi 28 kutokana na kipigo walichoipa JKT Oljoro cha mabao 3-0 leo kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Kabla ya hapo Azam FC ilikuwa inaongoza
ligi hiyo ikiwa na pointi 26, sawa na Mbeya City iliyokuwa katika nafasi ya
pili.
Lakini timu hizo mbili zimetoka sare ya
bao 3-3 leo kwenye Uwanja wa Chamazi Complex na kila moja zimebaki na pointi 27.
Maana yake, Azam FC inabaki katika
nafasi ya pili na Mbeya City tatu ikiwa ni tatu na zinatofautiana mabao ya
kufunga na kufungwa ‘GD’.
SImba inabaki katika nafasi ya nne ikiwa
na pointi 24 ilizofikisha baada ya ushindi wa jana wa mabao 4-2 dhidi ya
Ashanti United.
Katika mechi ya leo, mabao ya Yanga
yalifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 23, Mrisho Ngassa akaongeza bao
katika dakika ya 30 na Jerry Tegete katika dakika ya 54.
0 COMMENTS:
Post a Comment