Kocha Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic ‘Loga’ amesema mpaka kufikia sasa wakati timu
yake ikiendelea kujifua, mchezaji anayemuona kuwa na uhakika wa namba kwenye
safu ya ushambuliaji ni Uhuru Selemani.
Uhuru
ambaye amerejea klabuni hapo baada ya kuichezea Coastal Union kwa mkopo,
amekuwa akionyesha kiwango kizuri na kujituma katika mazoezi.
“Uhuru ni
mchezaji mzuri uwanjani, ndiye naona ana uhakika wa namba kwenye ushambuliaji,
labda sijui hapo baadaye kama atakuja kubadilika, lakini mpaka sasa ndiye
anaona ananifaa mbele,” alisema Loga.
Uhuru
alipelekwa Azam FC kwa mkopo kisha Coastal lakini kote alikuwa na wakati mgumu
wa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.







0 COMMENTS:
Post a Comment