December 2, 2013


Ashanti United ipo kwenye mikakati ya kuiwania saini ya kiungo wa zamani wa Simba na Yanga, Mohammed Banka kwa ajili ya kuiongezea nguvu timu hiyo kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.


Imeelezwa kuwa, Banka amemaliza mkataba wake na Bandari FC ya Kenya alikokuwa anacheza, hivyo yupo nchini kama mchezaji huru huku timu nyingi, ukiacha Ashanti, nazo pia zikiulizia huduma yake.
Chanzo makini kutoka ndani ya Ashanti kilisema timu hiyo inazungumza na mchezaji huyo ili iweze kuona kama itaweza kumpata.

“Kuna wachezaji wanawataka lakini kwenye orodha yao lipo pia jina la Banka na wanamtaka kutokana na uzoefu wake na mchango wake kwenye soka, kwa hiyo kwa sasa wanajaribu kufanya naye mazungumzo waone kama wanaweza kumnasa kwa sababu kuna timu nyingine pia zinamnyemelea,” kilisema chanzo hicho.


Katibu Mkuu wa Villa, Mbarouk Kasanda, amesema wameshafanya mazungumzo na kiungo huyo na kila kitu kinakwenda sawa, hivyo wana asilimia 80 za kumnasa.

“Kilichobaki ni saini yake tu lakini kila kitu kimekwenda kama kilivyopangwa, tumeshazungumza naye na yeye pia ameafiki, kwa hiyo uhakika wa kuwa naye kwenye mzunguko wa pili ni asilimia 80,” alisema Mbarouk.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic