December 2, 2013


Kocha Mkuu wa Simba, Zdravok Logarusic, amekutana na mchezaji wa kwanza wa Simba, kipa Yaw Berko, lakini akafanya kituko kwa kukagua tumbo lake hadharani.

Logarusic, raia wa Croatia, alifanya jambo hilo jana na kushuhudiwa na SALEHJEMBE, wakati akiwa na viongozi wa timu hiyo, kaimu makamu mwenyekiti, Swed Nkwabi na mjumbe wa kamati ya utendaji Said Pamba, wakati wakimuonyesha kocha huyo Uwanja wa Kinesi unaotumiwa na kikosi hicho kwa mazoezi.

Wakati Logarusic, maarufu kwa jina la Loga, akiwa ndani ya Uwanja wa Kinesi, alikutana na Berko ambaye naye ni kipa mpya wa Simba. Mara baada ya kumaliza kumsalimia, alifunua tumbo lake bila ruhusa ya kipa huyo akikagua jinsi alivyo fiti.

Loga awali alikuwa akizungumza na Nkwabi juu ya mipango ya kuanza mazoezi ya kikosi hicho ambapo wakati wakijadiliana juu ya kuwapelekea nyota hao gym, kocha huyo alisema hataki hilo lifanyike kwa sasa, ndipo alipoamua kufunua fulana ya Berko na kuangalia jinsi tumbo lake lilivyo.

Mara baada ya kumaliza kuliangalia tumbo hilo, akitumia sekunde mbili, Loga alimfunika na kusema siku zote anajua kuwa wachezaji wa Kiafrika wako sawa kimazoezi na kumwambia Nkwabi hakuna ulazima wa kuandaa mazoezi hayo.

“Unaona, nilikwambia najua kuwa wachezaji wa Kiafrika wako sawa, angalia jinsi tumbo la mazoezi lilivyo, nafikiri hiyo ratiba ya gym tuifute kwa sasa, tutaifanya huko mbele, kwa sasa nataka hayo tuliyoongea tukayafanye kwanza,” alisema Loga huku akiwaacha katika mshangao watu wote walioshuhudia tukio hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic