December 3, 2013

MENEJA UHUSIANO WA AIRTEL TANZANIA, JACKSON MBANDO AKIFAFANUA JAMBO KUHUSIANA NA DROO YA MIMI NI BINGWA.  KUSHOTO NI OFISA WA BODI YA MICHEZO YA KUBAHATISHA TANZANIA, ABDALLAH HEMED.

Kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania imetangaza washindi wa droo ya kwanza ya ‘Mimi Ni Bingwa’ inayolenga kuwazawadia wateja wake waaminifu.

Katika droo hiyo pia washindi wawili walizawadiwa safari ya kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United moja kwa moja (live) katika ligi kuu ya mpira w

Akizungumza wakati wa droo hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema droo hiyo imefuatia baada ya kampuni yake kuingia katika ushirikiano na klabu ya Manchester United wiki chache zilizopita.
“Leo hii tunatangaza washindi wa droo yetu ya kwanza ya promosheni ya ‘Mimi Ni Bingwa’. Tunaamini kuwa ushirikiano wetu na klabu ya Manchester United utawapa wateja wetu uzoefu mpya katika uangaliaji wa soka.
 “Bado kuna zawadi nyingi zitashindaniwa ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa ya Shilingi milioni 50. Kadri unavyoshiriki kwa kujibu maswali ndivyo utakapopata nafasi kubwa ya ushindi,” alisema Mmbando.
Alimtaja mshindi wa tiketi mbili kuwa ni Leonard Dickson Lyatuu, mkazi wa Njiro mkoani Arusha na kuongeza kuwa nafasi nyingine 13 na tiketi bado zitashindaniwa mwishoni mwa droo ya mwezi wa kwanza itakayomalizika katikati ya mwezi Desemba mwaka huu.
Pia aliwataja Harrison Wilson Mwambogola, mkazi wa Kigogo jijini Dar es Salaam na Stephen Asheri Chapile, mkazi wa Tengeru mkoani Arusha  waliojishindia shilingi milioni 5 kila mmoja na wateja wengine 20 ambao wamejishindia shilingi milioni moja (1) kila mmoja.

Washindi wengine walioibuka na zawadi ya shilingi milioni moja kila mmoja ni Tabu Nasiru,  David Geoffrey Mtitu, Fikiri Samuel Ndaki, Godfrey David Msiu, Dickson Victor Mjata, Joseph Dominic Mboya, Benezek Bahati Macha , Stephen Asheri Chapile, Bida Edwin Mwaisoloka, Rashid Jacob Kagombola, Joseph Steven Mambo, Harrison Wilson Mwambogolo,Andronice Constantine Lashayo, Abdi Ibrahim Mohammed

Mmbando alisema kuwa bado zawadi nyingi zaidi kushindaniwa na kuongeza kuwa ili kushiriki katika promosheni hiyo mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) ukiwa na neon “BINGWA’ kwenda namba 15656.

Aliongeza kuwa Airtel pia imeweka vituo maalum kwa ajili ya wapenzi wa Man U kuangalia mechi za Manchester United bure kupitia luninga kubwa, hususani katika maeneo ya Coco Beach huku wakipata burudani kabla na baada ya mechi.

Droo hiyo ilishuhudiwa na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic