EZEKIEL Kamwaga, Kaimu Ofisa Habari wa Klabu ya Simba amesema klabu hiyo inaendelea na mchakato wa kumtafuta Ofisa Habari kwani yeye ataondoka hivi karibuni kwenda nchini Uingereza.
Kamwaga alipewa nafasi hiyo kwa muda wa miezi miwili baada ya aliyekuwa kwenye nafasi hiyo Haji Manara kubwaga manyanga.
Wakati huu Manara yupo zake ndani ya Yanga akiwa kwenye kitengo cha Ofisa Habari.
Kamwaga amesema:-“Ninakaimu nafasi ya Ofisa Habari kwa muda wa miezi miwili, mwezi ujao nitakuwa naondoka Simba naenda UK, hivyo klabu itamtangaza Ofisa Habari mpya. Mchakato unaelekea kukamilika.
“Simba ni ile ile, mashabiki ni wale wale niliowaacha 2013, kilichobadilika sana Simba, imeanza kuwa klabu yenye watu wenye heshima zao, sasa hivi kuna watu kama akina Dr Janabi, akina Mo Dewji, Barbara. Lakini pia sasa kuna mabadiliko kwenye social media," .
Ameitendea haki nafasi yake ya ukaimu afisa habari ndani ya Simba inavyotakikana ahsante.
ReplyDeleteUpo sahihi kabisa ndugu yangu, hilo halina shaka. Pia nadhani kuwa na elimu (ya kutosha) ya kazi unayoifanya nalo ni jambo muhimu sana. Kwenye taasisi yoyote ile, bila kwenda shule kusomea kazi unayoifanya utabaki kuwa ni "professional" uchwara. Itafika mahali kazi itakushinda tu maana utakuwa huijui misingi halisi ya kazi yako.
DeleteWachangiaji mmeongea vizuri sana. Naongezea hapo kwenu kwamba kwa level ya juu ya weledi iliyofikia Simba katika muundo wa uongozi, benchi la ufundi, mafanikio y uwanjani kitaifa na kimataifa, kwa kweli wanahitaji afisa habari mwenye taaluma sahihi na weledi wa kutosha ambaye pia ni mtendaji makini ili anapohitaji katika matukio ya kazi yake, taarifa yake inakuwa inaeleweka kwa namna ya mpangilio wa uzungumzaji au uandishi na yenye tija kwa wadau wote wanaoifuatilia Simba nje na ndani ya nchi. Katika hili, ndugu yetu Kamwaga anaweza. Ana utulivu mzuri katika uzungumzaji wake, mpangilio wa maneno ya namna ya kufikisha ujumbe. Huu ndio mfano bora wa afisa habari wa timu kubwa kama tunavyoona kwa wenzetu Ulaya, Afrika kaskazini na Afrika Kusini. Kazi ya kuropoka, kupayuka, kukejeli, kukashfu, mihemko, n.k. waachiwe mashabiki. Kwa kiasi fulani, niliona afisa habari wa zamani wa Yanga Ndg. Dismas Ten alikuwa na weledi wa aina hii na pia Ndg. Hassan Bumbuli anaongea kwa utulivu na mpangilio mzuri kama asipovurugwa. Lakini Ndg. Kamwaga ana uwezo mkubwa sana na nasikitika kuona anaondoka. Alistahili kuwepo pale kama sehemu ya timu imara ya uongozi wa Simba yenye weledi na dira pana ( Vision & Mission) ya mafanikio.
DeleteIsitoshe, huyo vilevile ni muungwana
ReplyDeleteHongera Ezekiel Kamwaga, bila shaka unaenda BBC maana kuna siku walikutaja kama 'mwandishi wetu aliyepo Dar es Salaam', nikaona ukiripoti kama mwakilishi. Taaluma ni kitu muhimu kwa kila fani!
ReplyDeleteAnakimbia midomo ya koro fc hehehe
ReplyDeleteAna dili kubwa UK, usidhani wote wanawaza kushabikia mpira muda wote kama wewe. Ushabiki bila hela utakosa hata ya kiingilio
DeleteKamwaga ni mkonge ktk tasnia ya habari tunakujua ni simba oG, ruksa nenda Uk. Tuombee tupate msemaji wa character yako brow
ReplyDeleteKamwaga ni media professional halisi ambaye anaifanya kazi yake kwa kuzingatia maadili ya kazi.
ReplyDeleteYule mwendazake toka Simba kuna wakati alikuwa anaropoka hadi unaona matamshi yake ni kinyaa na unashindwa kuelewa kama huyu mwendazake alipata kusomea angalau kupata basic certificate ya mass media communication.Waandishi wa habari, watangazaji inabidi Media association yenu mliinde na kuipigania tasnia yenu badala ya kuacha kila anayemkaa toka usingizini ni kuwa naye ni media proffesional.