BAADA ya Yanga kuridhia kutumongezea mkataba mpya Antonio Nugaz ambaye amehudumu kwa muda wa miaka miwili katika nafasi ya Uhamasishaji ameandika ujumbe wa kuwashukuru Yanga.
Kupitia Ukurasa wa Instagram Nugaz ameandika namna hii:-"Kwa udhati wa moyo wangu naomba niwashukuru kuanzia uongozi wote wa Yanga chini ya mwenyekiti wetu Dk. Mshindo Mbette Msolla na Kaimu Katibu Mkuu Mpya Senzo Mbatha Mazingiza, wafanyakazi wenzangu wote kwa upendo wenu kwa kipindi chote cha miaka miwili niliyoitumikia Yanga kwa moyo mkunjufu na kujitoa kwangu.
"Mungu awabariki, awalinde na awape kila hitajio la nafsi zenu ili tuweze kuipeleka mbele brand, (nembo) ya Yanga.
"Wanachama,wapenzi na mashabiki wa Yanga ninyi mmekuwa na mimi kwa moyo mmoja ahsanteni sana. Nawapenda sana na niatendelea kuwa nanyi.
"Tutaonana tena hivi karibuni. Insha Allah,".
Huyu anajielewa, sio yule jamaa
ReplyDeleteNugaz watu Simba tunajua wewe ni Yanga lakini kwa huu uweledi uliuonesha basi tunakukaribisha kwenye simba day.Hujakosea hata kidogo kumwita Kahaji Manara msukule ni msukule hasa yule hamna kitu pale,wanayanga watakuelewa muda si mrefu.
DeleteUko sahihi kbs ndugu yangu, sina la kuongeza hapa!
DeleteYanga kuna fukuta mtokoto huu mlipuke ni hatari..kwa jinsi tunavyoijua Yanga kocha yupo hatarini kufukuzwa.
DeleteAda ya mja hunena muungwana ni kitendo. Tofauti ya mshenzi na mstaarabu.
ReplyDeletePamoja sana nugaz
ReplyDeleteHuwezi kumsafisha nguruwe akawa msafi.Kwani uchafu ndio maumbile yake.Nugaz amemuonyesha Msukule ustaarabu ni nini?
ReplyDeleteMwenye hekima utamtambua kwenye matendo
ReplyDeleteNakutakia kila la heri ndugu Nguwaz na wakati ule ule nalinganisha reaction zako na zile za yule aliechukuwa cheo chako baada ya kuenguliwa. Kwahakika umepokea kwa unyenyekevu mkubwa bila ya panic au kulumbana na hivo ndio inavohitajika katika uhai. Mmekaa jwa amani na mnatokana kwa aman kwa sababu ikiwa jicho kwa jicho dunia nzima itapata upofu
ReplyDeleteBila ya shaka hawachi kuona uchungu, lakini aliyameza na hakuikashifu wala kumwaga siri za timu yake
ReplyDeleteWaandishi chokochoko zenu hazikusaidia kitu. Mliandika Nugaz afukuzwa kumbe kamaliza mkataba wa utumishi wake. Mlitaka apande jazba ili afoke lkn kwavile anajielewa na anaelewa maana halisi ya kwisha kwa mkataba wake hakufoka wala hakupwaga. Nina imani uongozi wa Yanga umemuandalia Nugaz nafasi nyengine ya kwenda kuhudumu ndio maana akamalizia shukran zake kwa kusema tutaonana hivi karibuni.
ReplyDeleteTutege masikio kusikiliza in shaa Allah.