September 12, 2021


WAWAKILISHI wa Tanzania, Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika leo wameanza kwa kupoteza mchezo wa awali hatua ya Ligi ya Mabingwa wakiwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwa kuwa ilikuwa ipo nyumbani ila ghafla mambo yalikuwa ni mazito.

Dakika 45 zilikamilika kwa timu zote kutoshana nguvu jambo ambalo liliwafanya waende kenye vyumba vya kubadilisha nguo ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 0-0 Rivers United .

Kipindi cha pili ngoma ilipinduka baada ya Rivers United kuongeza kasi ya mashambulizi na kupata kona ya kwanza dakika ya 50 iliyoleta bao lililopachikwa na nyota wao Moses Omdumuke .

Ilikuwa ni kichwa kilichomshinda kipa namba moja Diarra na kuwafanya Rivers United kusepa na ushindi.


Jitihada za Yanga kupitia kwa mshambuliaji wao Heritier Makambo ambaye alimpisha Ditram Nchimbi hazikuweza kuleta matunda na kuwafanya wapoteze furaha katika mchezo wa kwanza.

Yanga ina kazi ya kwenda kusaka ushindi nchini Nigeria kwenye mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa unaotarajiwa kuchezwa Septemba 18.

10 COMMENTS:

  1. Mm nimejuwa watashinda sababu wamemsajiri manara

    ReplyDelete
  2. Nawasalimia kwa Jina la gundu la Manara wacha liendelee ndani ya Yanga mnatakiwa kuitikia vichapo wacha viendelee kwa wananchi mpaka wamfukuze kocha na CV yake fake.
    Zile kejeli za kwamba Simba walibahatisha ligi ya mabingwa sasa kimya. Mpira sio porojo na hekaya za Manara.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba walibahatisha? Ni wivu tu ndio unawasumbua watu. Kubahatisha huwa ni kitu cha mara moja, lkn kwa anayefuatilia mpira muda mrefu (na pia mwenye akili timamu) hawezi hata kuropoka kwamba Simba ilibahatisha, maana kufikia hapa hii imekuwa ni process ya muda mrefu. Recent CAF rankings zinaanika wazi kwamba kwy 'top 40' ya ubora Africa Simba ni ya 14, na namba 40 inakamilishwa na Zanaco ya Zambia. Kwy hizi 40 kuna timu hazipo kbs ktk list hii, hata ukitumia torch kuzitafuta! Bado utasema Simba inabahatisha! Na uzuri wa rankings za CAF huwa hazitengenezwi na Karia au TFF. Kwa ujumla wivu na hasad ni mambo mabaya sana na hata dini zinakemea mambo haya. Kinachotakiwa ni "wivu wa maendeleo", ili nawe uchukue hatua stahiki kufikia maendeleo ya mtu mwingine, vinginevyo watu watabaki kujinasibu tu lkn hawatakuwa na lolote jipya zaidi ya kuendeleza tu wivu kwa Simba.

      Delete
  3. The return of Champions! Lauli mbiu zinalipa ukiwa na timu nzuri na maandalizi mazuri, vinginevyo ni porojo tu!

    ReplyDelete
  4. Kipa anadaka mishale Ila mpira hauoni

    ReplyDelete
  5. Bado goli 4.Na huyu Msukule aache tabia ya kuwacheka Utopolo chooni sio ustaarabu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic