December 10, 2013

NJOVU (KULIA) AKIWA NA MANJI, LEO.



YANGA imemtangaza Beno Njovu katibu mkuu wa klabu hiyo kongwe.

Kwa sasa nafasi hiyo anaikaimu Lawrance Mwalusako, beki wa zamani wa Yanga.
Kabla ilikuwa inashikiliwa na Selestine Mwesigwa ambaye aliondolewa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuph Manji kwa kutoridhika na utendaji kazi wake klabuni hapo.
Njovu ametangazwa leo na Maji kwenye makao makuu ya klabu hiyo. Kawaida nafasi hiyo ni ya kuajiriwa.
Manji alisema uamuzi wa kumteua Njovu katika nafasi hiyo umefikiwa na kamati ya utendaji.
Aidha, alisema kuwa Njovu ameanza kazi rasmi jana mara baada ya kutangazwa kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Kariakoo jijini Dar na kwamba atakabidhiwa Ofisi na Mwalusako Januari 19, mwakani siku ya Mkutano Mkuu wa klabu hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic