SEIF Ahmed ‘Magari’ ametangazwa kuwa
Mwenyekiti wa Kamati ya Michuano ya Kimataofa.
Magari ambaye amekuwa jembe la Yanga
katika usajili kwa kuwa ni mjumbe wa kamati ya usajili, ametangazwa leo na
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.
Manji amesema Magari atafanya kazi ya
kuteua wajumbe ambao wataunda jopo la kamati yake hiyo.
“Magari atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Michuano ya Kimataifa ambaye hapo baadaye atawataja wajumbe atakaokuwa nao
kwenye kamati yake hiyo,” alisema Manji.
Kupitia kamati hiyo, Magari ataongoza
kazi ya kuratibu zoezi zima la maandalizi katika mechi za kimataifa za Yanga.
Yanga ndiyo wawakilishi wa Tanzania
katika michuano mikubwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika.








0 COMMENTS:
Post a Comment