Timu ya Tanzania Bara imeshindwa kufika
fainali baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji Harambee Stars.
Katika mechi iliyokuwa inapigwa kwenye
Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi na Kili Stars kushindwa kufurukuta.
Bao la Clifton Miheso katika dakika ya 4
baada ya kipa Ivo Mapunda kuupangua mpira, liliizamisha Stars ambayo haikucheza
vizuri.
Juhudi za Stars kusawazisha bao hilo
bila ya mafanikio huku safu yake ya ulinzi ikihaha kuwazuia Miheso na Allan
Wanga.
Kutokana na ushindi huo, Kenya sasa
itaivaa Sudan na Stars itaivaa Zambia kwa mara ya pili kutafuta mshindi wa
tatu, mechi zitapigwa Alhamisi.







0 COMMENTS:
Post a Comment