Makipa wawili wa Yanga, Juma Kaseja na
Mustapha Ally ‘Barthez’ wameonyesha ushirikiano mkubwa mazoezini.
Kocha wa makipa wa Yanga, Razak Siwa
amesema Kaseja na Barthez wameonekana si wageni kikazi.
“Wanashirikiana vizuri sana, hii
inaonyesha ni watu waliofanya kazi pamoja hapo awali.
“Hiki ni kitu kizuri na matumaini
makubwa kwamba mambo yatakwenda vizuri zaidi,” alisema Siwa.
Kaseja na Barthez, pamoja wamewahi
kufanya kazi wakiwa Simba.
Lakini Barthez alitua Yanga, kabla ya
Kaseja naye kurejea Yanga katika dirisha dogo.







0 COMMENTS:
Post a Comment