Kocha mpya wa Simba, Zdravko Logarusic
ameeleza maana ya jina lake kuwa ni mtu mwenye afya njema.
Akizungumza leo katika mazoezi ya Simba,
Logarusic amesema jina la Zdravko ndiyo lenye maana hiyo.
“Lakini hili la Logarusic sijui hata
maana yake, nahisi litakuwa ni jina tu la kawaida,” alisema.
“Hili la kwanza ni kati ya majina
yanayovutia kabisa duniani na wengi wanalipenda.”
Kocha huyo ambaye anapenda utani lakini
siriaz anapokuwa kazini, aliendelea na kazi ya kukinoa kikosi cha Simba kwa
mara ya pili.
Baada ya kusaini mkataba wa miezi sita,
jana alianza kukinoa kikosi chake kwa mara ya kwanza.







0 COMMENTS:
Post a Comment