Manchester United
imefanikiwa kuichapa Shaktar kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi ya mabingwa
Ulaya.
Bao la United limetupiwa
kimiani Phil Jones lakini kali zaidi ni Man City kuichapa Bayern Munich 3-2
ikiwa kwao Munich, Ujerumani.
Ingawa Bayern walitangulia
lakini City walizinduka na kusawazisha mabao yao kupitia David Silva, Kilarov
na James Milner akamaliza kazi.
Cristiano Ronaldo naye
amerejea uwanjani na kusaidia Real Madrid kuichapa Copenhagen kwao kwa mabao
2-0, yeye akifunga la pili lakini Luka Modric ndiye alifungua mlango kwa bao la
kwanza.
Dakika ya 89, Ronaldo
angeweza kufunga bao la pili la mkwaju wa penalti aliopiga haukuzaa bao.
Matokeo mengine:
PSG walilala kwa mabao 2-1
kutoka kwa wenyeji wao Benfica licha ya kutangulia na bao la Cavani. Vicktoria
Plzen 2-CCSKA 1, Real Sociedad 0, Bayer Leverkusen 1.
Mechi kati ya Galatasaray
dhidi ya Juventus imeahirishwa kutokana na barafu kujaa uwanjani.
Juhudi za kuziondoa barafu
hizo hazikuzaa matunda na mwisho ikatangazwa kuahirishwa kwa mechi hiyo.







0 COMMENTS:
Post a Comment