Wachezaji saba raia wa Nigeria juzi
walitua kwenye mazoezi ya Ashanti United yanayofanyika kwenye Uwanja wa
Msimbazi Rover, Ilala, Dar, kwa nia ya kusajiliwa klabuni hapo.
Wanigeria hao waliungana na wachezaji
wengine ambao nao kwa mara ya kwanza wanafanya mazoezi na timu hiyo yenye
maskani yake maeneo ya Ilala jijini Dar ambao ni wachezaji wawili wa zamani wa
Simba, Juma Jabu na Mohammed Banka, walio kwenye mazungumzo na timu hiyo.
Mara baada ya kuisha kwa mazoezi hayo
yanayofanyika majira ya jioni hivi.
Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Nico
Kiondo, alisema wageni hao hawana nafasi klabuni hapo kutokana na viwango vyao
duni.
“Ni wachezaji wenye viwango vya kawaida
sana, hatuna haja ya kuwachukua kwa sababu hapa nyumbani tuna wachezaji wenye
viwango vizuri zaidi yao na sidhani kama watakuja tena, nafikiri Kocha Kibadeni
(Abdallah) ameshazungumza nao juu ya viwango vyao ukilinganisha na watu
tunaowahitaji.
“Lakini Banka na Jabu bado tunaendelea
kuwaangalia tukiwa bado tunazungumza nao kwa ajili ya mzunguko wa pili” alisema
Kiondo.
.jpg)







0 COMMENTS:
Post a Comment