December 10, 2013



 
OLOYA KAZINI VIETNAM
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, Sredojevic Milutin ‘Micho’ amesema Moses Oloya au Emmanuel Okwi wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa Yanga hasa katika Ligi ya Mabingwa afrika.


Kumekuwa na taarifa kuwa Yanga imekuwa ikiwafuatilia Waganda hao huku ikitaka kumchukua mmoja wao kutokana na mazungumzo yao yatakavyokuwa.
 
Akizungumza na SALEHJEMBE, Micho alisema wachezaji hao wawili wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa aina ya uchezaji wa Yanga.
 
OKWI ALIPOKUWA ETOILE DU SAHEL YA TUNISIA
“Nimeona Yanga inacheza kwa kasi, pia mabeki wanapita au mawinga wanapiga krosi.

“Ukiwa na wachezaji kama Okwi au Oloya kwa mfumo huo, msaada unakuwa mkubwa sana.

“Kweli nimesikia wanawafuatilia na iwapo wakimpata mmoja wao, basi watakuwa msaada kwao,” alisema.

Kuhusiana na kuvuliwa ubingwa na Tanzania Bara, Micho alisema The Cranes hawakuwa makini.

“Tulipoteza nafasi nyingi na kufanya uzembe kwenye safu ya ulinzi. Mwisho tulistahili adhabu,” alisema.

Kili Stars iliing’oa Uganda kwa mikwaju ya penalti 3-2 ikiwa ni baada ya sare ya mabao 2-2 katika mechi ya robo fainali ya michuano ya Chalenji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic