Kilimanjaro Stars imefanikiwa kufuzu katika hatua ya
nusu fainali ikiwa ni pamoja na kuivua ubingwa, Uganda, The Cranes.
Katika mechi iliyomalizika punde katika michuano ya
Chalenji inayofanyika nchini Kenya, Stars imevuka kwa mikwaju 3-2 huku kipa Ivo
Mapunda akiwa shujaa.
Ivo alifanikiwa kudaka mikwaju miwili ya penalty, akianza kudaka wa Alucho kabla ya
kudaka ya pili iliyopigwa na Sserunkuma anayecheza naye katika kikosi kimoja
cha mabingwa wa Kenya, Gor Mahia.
Okwi na Kiiza walipata upande wa Uganda, lakini
upande wa Stars, Samatta na Nyoni wakakosa. Waliofunga ni Kiemba, Yondani na
Chuji.
Katika dakika 90 timu hizo zilitoka sare ya bao 2-2,
Stars wakianza kuongoza kwa mabao mawili ya Ngassa, lakini Uganda wakasawazisha
kupitia Sserunkuma (Dk ya 16) na Martin Mpuga (dk73).
0 COMMENTS:
Post a Comment