January 8, 2014


Kocha aliyetimuliwa Yanga, Ernie Brandts amechukua uamuzi wa kuondoka nchini kimyakimya.

Brandts aliondoka nchini juzi usiku na kuwasili nchini Uholanzi jana asubuhi.


Alipoulizwa sababu ya kuondoka kimyakimya huku akiwa ametangaza ataondoka usiku, Brandts alisema anaamini wazo lake lilikuwa zuri kiusalama.


“Sijui kwa nini nimekuwa na hofu, lakini nimeona hivi ni sahihi.
“Nashukuru niko hapa uwanja wa ndege na ninaondoka kurejea nyumbani.

“Mke na mtoto wangu wananihitaji na ninaamini kipindi hiki ndiyo bora cha kurejea nyumbani na kuwa pamoja na familia yangu,” alisema.

Brandts aliipa Yanga ubingwa na hadi anafukuzwa, Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara wakifuatiwa na Azam FC.
Alifukuzwa baada ya kikosi chake kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mechi ya Bonanza la Nani Mtani Jembe iliyopigwa Desemba 21, mwaka jana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic